1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shule zafunguliwa upya Gaza

Oumilkher Hamidou24 Januari 2009

Umoja wa Ulaya wapanga kuanza haraka kuijenga upya Gaza

https://p.dw.com/p/GfVi

Gaza:

Shule zaidi ya 200 za Ukanda wa Gaza zinazogharimiwa na Umoja wa mataifa zimefunguliwa upya hii leo-kwa mara ya kwanza tangu mpango wa kuweka chini silaha ulipokomesha wiki tatu za hujuma za Israel dhidi ya Hamas.

Wanafunzi laki mbili wanakwenda katika shule 221 zinazogharimiwa na shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi wa kipalastina .Wakati huo huo muakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana amesema jumuia yao inapanga kuanza haraka shughuli za kuijenga upya Gaza.Na Ufaransa imetuma manuari yenye kubeba helikopta katika fukwe za Gaza ili kuzuwia biashara ya kichini chini ya silaha zinazoingizwa katika eneo hilo linalosimamiwa na Hamas.