1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siemens kufuta nafasi 6,800 za kazi nchi mbali mbali

27 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DDuz

MUNICH:

Kampuni kubwa ya Kijerumani-Siemens-imethibitisha kuwa nafasi 6,800 za kazi zitafutwa katika kitengo cha mawasiliano ya simu kote ulimwenguni katika juhudi ya kuharakisha mpango wake wa mageuzi.Nchini Ujerumani pekee,hadi watu 2,000 watapoteza ajira na kama 1,200 wengine watahamishwa katika idara zingine. Siemens inajaribu kuliuza tawi lake la mawasiliano ya simu SEN lililopoteza masoko kwa sababu ya ushindani wa simu zinazopigwa kwa njia ya mtandao.