1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SIERRA LEONE : Wagombea urais wadai kuongoza matokeo

10 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBR0

Vyama vya wagombea wawili katika marudio ya uchaguzi wa rais nchini Sierra Leone vyote vinadai kuongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi huo wakati nchi hiyo ya kimaskini ilioathiriwa na vita ikisubiri matokea rasmi.

Kwa mujibu wa nusu ya matokeo hayo kutoka zaidi ya theluthi moja ya vituo vya kura mgombea wa upinzani Ernest Koroma wa chama cha APC alikuwa mbele ya mpinzani wake Makamo wa Rais Solomon Berewa wa chama tawala cha Sierra Leone SLPP.

Kwa mujibu wa Ransford Wright mratibu wa Mtandao wa Radio Huru IRN ambayo inajumuisha vituo 20 vya radio vyenye kutangaza matokeo yasio rasmi mwendo wa matokeo hayo hadi sasa unaonyesha kwamba mgombea wa APC anaoongoza kwa asilimia 54.5 wakati wa chama tawala cha SLPP akiwa ana asilimia 45.5.

Matokeo rasmi ya marudio ya uchaguzi huo wa rais yanatarajiwa kuanza kupatikana usiku wa manane leo hii.