1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kifua kikuu Duiniani.

23 Machi 2007

Leo ni siku dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu duniani.Ugonjwa huu wa kifua kikuu umeripotiwa kuua zaidi ya watu millioni moja unusu barani Afrika kupeleka hali duni za makaazi yao kwenye maeneo ya mdongo poromoka.

https://p.dw.com/p/CB56

Mada ya mwaka huu ya kutathmini maradhi ya kifua kikuu ni, ''kuwepo kwa ugonjwa kifua kikuu popote ni kuwepo kwa ugonjwa wa kifua kikuu kila pahali duniani''. Na kwa jinsi unavyosambaa kwa haraka kupitia hewa,ndivyo unavyozidi kuwa kitisho kwa ulimwengu hasaa barani Afrika. Shirika la Medecines San Frontiers,limesema maeneo ya madongo poromoka ambapo kuna msongamano mkubwa wa watu,ndipo ugonjwa wa kifua kikuu husambaa kwa haraka.

Christien Genevier,kiongozi wa shirika la Medecine San Frontiers nchini Kenya alisema, ''awakuta watu wasita wanaishi katika nyumba moja ambayo haina madirisha ya kutosha,asilimia 80 ya wagonjwa tunaotibu wanaishi hivi,na hali hiyo husababisha mkurupuko wa maradhi ya kifua kikuu''

Kadhalika,ukosefu wa madawa muafaka kumesababisha wagonjwa kushindwa kutibiwa na madawa ya kisasa. Hali hii humshurutisha mgonjwa huyo kutumia mchangayiko wa madawa mengi hata tembe 30,yanayomfanya kutapika na kuhara.

Hali hii imesababisha dadi ya wagonjwa kuongezeka kila siku,kwa mfano kituo kimoja cha matibabu huko Mathare Kenya,hutibu watu mia sita walio na kifua kikuu.Wengi wao wanaugua maradhi ya ukimwi,na madawa ya kisasa yanaposhindwa kuwapa nafuu,madakitari wanalazimika kutumia mchanganyiko wa dawa yanayoitwa MDR-TB. Na asilima 45 ya wagonjwa wanokunywa madawa haya kwa kipindi cha miezi 18 hadi 24 hufariki kabla kupona.

Kwengineko Afrika Kusini, aina ya maradhi ya kifua kikuu inayoonekana nchini humo sasa imedhihirika katika mataifa tajiri kama Ulaya,Marekani na Canada. Shirika la afya duniani WHO limesema aina hii ya kifua kikuu XDR-TB,ni ile ambayo madawa ya kisasa na yale ya zamani hayawezi kuidhibiti kirahisi. Mkurugenzi wa mpango wa STOP TB Mario Raviglione,amesema hali hii imeonekana katika nchi 35 na ni kitisho kikubwa kwa ulimwengu.

Shirika la afya duniani,limesema watu millioni moja unusu wanaugua maradhi ya kifua kikuu ulimwenguni,kila mwaka zaidi ya watu laki nne huambukizwa maradhi haya na laki moja hufariki kila mwaka.

Tatizo kuu ni kwamba huku baadhi ya serikali ulimwenguni zikikabiliana na maradhi haya vilivyo,serikali zengine zimebakia nyuma na kusababisha mapambano dhidi ya ugonjwa huu kuwa kibarua kigumu. Kwani ikiwa mtu mmoja atatibiwa katika nchi mmoja na mwengine anayeugua kusafiri katika nchi hiyo,anawaambukiza wenzake upya.

Isabella Mwagodi