1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SIKU YA KIFUA KIKUU

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFp

NAIROBI:

Leo ni siku ya kupiga vita kifua kikuu:Kiasi cha wakenya 13 wanafariki dunia kwa saa kwa kuugua kifua kikuu –mkuu wa shirika la afya la kitaifa amearifu leo.Allan Ragi, mkurugenzi mkuu wa shirika la KANCO –muungano wa jumuiya hadi 850 alisema Kenya imejitokeza mbele mbele kabisa katika eneo hili kwa maradhi ya kifua kikuu kutokana na mipango yake mibaya ya kupambana na kifua kikuu.

Zaidi ya waafrika milioni 1 wanafariki dunia kila mwaka kutoka na TB-kifua kikuu.Ragi alisema nchi jirani kama Uganda zinakabiliana bora zaidi na maradhi haya kuliko Kenya.