1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ujerumani atoa mwito wa mshikamano

Abdu Said Mtullya1 Desemba 2009

Watu duniani kote waadhimisha siku ya ukimwi lakini shirika la afya WHO lataka dawa aina ya "satavudine" iondolewe hatua kwa hatua

https://p.dw.com/p/KmVM
Waziri wa afya wa Ujerumani Philipp Rösler ametoa mwito wa kushikamana na wenye ukimwi.Picha: AP

Berlin.

Katika kuadhimisha siku ya ukimwi duniani leo, waziri wa  afya wa Ujerumani Philipp Rösler ametoa mwito  wa kujenga mshikamano na watu  wenye  maradhi hayo.Waziri Rösler   amesema  watu wanaougua maradhi ya ukimwi hawana haja  ya kuona haya au kuficha maradhi yao.

Hatahivyo waziri huyo amesisitiza umuhimu  wa kinga  kwa  kuwa  bado tiba haijapatikana.

Katika kuadhimisha siku ya leo, madaktari na mashirika  ya afya pia yametoa mwito wa kutenga fedha zaidi,kutoa elimu , na huduma  za kuwalinda wanawake vizuri zaidi dhidi ya maambukizi.

Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani,WHO limezitaka nchi zianze kuiondoa dawa ya ukimwi  "Stavudine" hatua kwa  hatua kwa  sababu inasababisha   madhara ya muda mrefu yasiyoweza  kuondolewa.

Madhara hayo ni pamoja na kudhoofika na kupagaranyika kwa mishipa  ya fahamu.