1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SOCHI : Merkel na Vladimir wataka amani Mashariki ya Kati

22 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYu

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Vladimir Putin wa Urusi wameunga mkono kukufuliwa kwa juhudi za amani Mashariki ya Kati za kundi la pande nne.

Kufuatia mazungumzo yao katika mji wa kitalii wa Bahari Nyeusi wa Sochi nchini Urusi viongozi hao wamesema mkutano uliopangwa kufanyika mjini Washington mwezi ujao wa pande hizo nne utatowa msukumo mpya kwa mchakato huo wa amani.

Kundi la pande hizo nne linajumuisha Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya,Urusi na Marekani.

Putin pia amemuhakikishia Merkel kwamba Urusi itaendelea kubakia kuwa msambazaji wa nishati wa kuaminika kwa Ulaya. Uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi umedhoofika tokea Urusi ilipofunga kwa muda bomba la kusafirisha mafuta kwa Ulaya wiki mbili zilizopita.

Hii ni ziara ya kwanza ya Merkel kwa Urusi tokea Ujerumani ishike wadhifa wa Urais wa Umoja wa Ulaya halikadhalika ule wa Kundi la Mataifa Manane yenye Maendeleo Makubwa ya Viwanda Duniani.