1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sofia. Brazil na Bulgaria kuchagua rais leo.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCy7

Uchaguzi wa rais unafanyika nchini Bulgaria na Brazil pia hii leo.

Mgombea ambaye ndie rais wa sasa Msoshalist Georgi Parvanov anaonekana kupata ushindi nchini Bulgaria, ambako upigaji kura tayari umeanza.

Wakati huo huo , kura ya maoni inaonesha kuwa rais Luiz Inacio Lula da Silva ananafasi kubwa ya kushinda kipindi kingine cha utawala nchini Brazil, licha ya madai ya ulaji rushwa dhidi yake.