1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Soko la ajira laimarika Ujerumani

3 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cjsg

NUREMBERG

Soko la ajira nchini Ujerumani limezidi kuwa bora hapo mwezi wa Desemba kuliko ilivyokuwa ikitegemewa kutokana na ukuaji mzuri wa uchumi.

Shirika la ajira lenye makao yake mjini Nuremberg limesema kwamba kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Ujerumani nchi ambayo ina nguvu kubwa kabisa za kiuchumi Barani Ulaya mwezi uliopita kilishuka kwa watu 78,000 na kuwa na kama watu milioni 3.5 sawa na asilimia 8.1 ikilinganishwa na asilimia 9.6 kwa mwaka juzi.