1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somaliland yafanya uchaguzi

13 Novemba 2017

Wananchi wa Somaliland, jimbo lenye utawala wake wa ndani lililojitenga na Somalia, wanafanya uchaguzi wa rais unaofanyika kila baada ya miaka mitano. Ni mara ya tatu kwa jimbo hilo kuandaa uchaguzi.

https://p.dw.com/p/2nXzd
Somaliland
Picha: DW/J. Jeffrey

J3 13.11 Somaliland Analysis - MP3-Stereo

Jimbo hilo ambalo zamani lilikuwa koloni la Waingereza lilijipatia uhuru wake mwaka 1960 lakini siku kadhaa badae likajiunga na Somalia na kuwa nchi moja ingawa mwaka 1991  baada ya miaka kadhaa ya mivutano mikubwa na serikali kuu mjini Mogadishu, Somaliland ikajitangazia  uhuru na kujitenga  Somalia.Uhuru huo lakini hautambuliwi kimataifa. DW imezungumza na mchambuzi wa kisiasa Ahmed Rajab kuhusu uchaguzi huo na kwanza anaeleza ni mambo gani hasa yanayoifanya Somaliland kuwa tafauti na Somalia hasa kwenye suala la kufanya uchaguzi kwa njia ya amani na ya kidemokrasia.