1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SPD yamchagua Olaf Scholz kugombea ukansela

Lilian Mtono
10 Mei 2021

Waziri wa fedha wa Ujerumani Olaf Scholz amechaguliwa na chama chake cha Social Democrats, SPD kugombea ukansela huku akiapa kuongeza kima cha chini cha mishahara iwapo watashinda uchaguzi mkuu wa mwezi Septemba.

https://p.dw.com/p/3tB0V
Deutschland Online-Bundesparteitag der SPD in Berlin - Olaf Scholz, Bundesfinanzminister und Kanzlerkandidat der SPD
Picha: Florian Gaertner/photothek/imago images

Waziri huyo wa fedha wa Ujerumani Olaf Scholz ameapa kuongeza kima cha chini cha mishahara baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Septemba, akiwa na matumaina ya kupata uungawaji mkono wa karibu watu milioni 10 wanaolipwa kima cha chini, kukisaidia chama chake cha Social Democrats, SPD kutoendelea kupata matokeo mabovu. 

Scholz ametoa ahadi hiyo kwa wajumbe wa chama hicho cha SPD waliompigia kura kugombea nafasi ya ukansela kutoka chama hicho cha siasa za wastani za mrengo wa shoto cha SPD. Meya huyo wa zamani wa Hamburg ameidhinishwa kwa asilimia 96.2 ya kura karibu 600 za wajumbe wa SPD, katika uchaguzi uliofanyika kwa njia ya mtandao mjini Berlin jana Jumapili.

Alisema "Kila kazi ina hadhi yake, kila kazi inastahili kuheshimiwa. Na hii ndio hasa inaakisi kiwango cha chini cha mshahara. Kisheria kiwango cha cha chini cha mshahara ni angalau € 12 kwa saa, kimepitwa na wakati."

Uchunguzi wa maoni katika siku za karibuni umeonyesha chama chake kimekuwa nyuma ya vyama vya watetezi wa Mazingira ama Greens na vyama vya kihafidhina vya kansela Angela Merkel, lakini pia kikitabiriwa kushindwa vibaya kwenye uchaguzi.

Chama cha SPD kilijiunga bila ya kusita na muungano wa serikali ya vyama vya kihadhidhina ya kansela Merkel baada ya uchaguzi wa mwaka 2017, licha ya upinzani mkali kutoka kwa wanachama wake waliokuwa na hofu kwamba muungano huo wa mara ya tatu na Merkel huenda ukaathiti msimamo wa chama hicho juu ya wafanyakazi.

Die Kanzlerkandidaten zur Bundestagswahl 2021.
Wagombea watatu kwenye nafasi ya ukansela, kutoka kushoto Armin Laschet wa CDU/CSU, Annalena Baerbock wa Greens na Olaf Scholz wa SPDPicha: Malte Ossowski/SVEN SIMON/picture alliance

Tafiti zina maoni tofauti kuhusu ushindani wa vyama hivyo.

Baadhi ya tafiti za maoni zimeonyesha kwamba chama cha watetezi wa mazingira kuwa mbele ya vyama vya kihafidhina vya Merkel, ambavyo pia vinajiandaa kupata pigo kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa katika uchaguzi ujao wa Septemba 26, kutoka kwa wapiga kura waliogadhabishwa na namna serikali ilivoyshughulikia janga la vitrusi vya corona kuanzia hatua za kufunga shughuli hadi mchakato mzima wa utoaji wa chanjo ambao umekuwa wa taratibu mno.

Tafiti nyingine hata hivyo zimeonyesha vyama hivyo vikikabana koo.

Kwenye kampeni za uchaguzi wa bunge, Scholz alijikita kwenye kuuza sera za mabadiliko ya kiuchumi miongoni mwa jamii na kuleta pia mabadiliko kwenye masuala ya mazingira, huku akiweka malengo ya kufikia mabadiliko hayo angalau ifikapo mwaka 2045. Scholz pia alijinadi kwa kujaribu kujitenga na mgombea wa chama cha Greens Annalena Baerbock kwa kuangazia enzi yake akiwa serikalini, na namna alivyikuwa akikosolewa kwa kukosa uzoefu.

Katibu mkuu wa chama hicho Lars Klingbeil amevielezea vyama vya kihafidhina vya Merkel kuwa vilivyogubikwa na mzozo mbaya kabisa wa kimamlaka sambamba na kashfa mpya zinazoibuka kila wiki, huku akikosoa chaguo la mgombea wao Armin Laschet, akielezea kwamba tayari limeashiria anguko la vyama hivyo.

Tizama Picha:

Amesema mgombea wao Scholz anasimamia malengo manne muhimu ambayo ni pamoja na kusimamia upunguzwaji wa usambazaji wa hewa ukaa ifikapo angalau mwaka 2045, kuimarisha mfumo bora kabisa wa usafirishaji barani Ulaya, uhuru wa kidijitali na mfumo imara wa huduma za afya.

Tafiti za maoni za hivi karibuni, zinaiweka SPD nyuma ya vyama ndugu vya CDU/CSU kwa takriban asilimia 16 huku watetezi wa mazingira wakiongoza kwa asilimia 26 ya kura.

Mashirika: RTRE/DPAE