1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Spian yaitoa Itali

23 Juni 2008

Spain ilivunja jana mwiko na kuilaza Itali ili kukata tiketi yake ya nusu-finali ya kombe la Ulaya.

https://p.dw.com/p/EPKL
Luca Toni .hakutamba.Picha: Reuters/Michael Kooren

Spian imekata tiketi yake ya kwanza ya nusu-finali ya kombe la Ulaya baada ya kuwapiku mabingwa wa dunia-Itali katika changamoto ya mikwaju ya penalty kwa mabao 4-2.

Russia nayo iliipiku Holland kimkakati na kimchezo na sasa ina miadi na Spain alhamisi ijayo .

Taifa Stars-Tanzania yazabwa mabao 2-1 na simba wa nyika Kamerun katika kinyan'ganyiro cha kanda ya Afrika ya kombe la dunia na leo mashindano mashuhuri ya Tennis ya Wimbledon yaanza-Je, Roger Federer atatamba na kutwaa taji lake la 6 ?

Timu 4 zitakazocheza nusu-finali ya kombe la Ulaya kati ya wiki hii zinajulikana sasa:Ujerumani itapambana na Uturuki jumatano hii na Spain iliowatimua jana mabingwa wa dunia Itali kupitia changamoto za mikwaju ya penalty kwa mabao 4:2 ina miadi na Russia, iliolipiza kisasi cha kulazwa na holland katika finali ya kombe hili la ulaya,mjini Munich, 1998.

Mabingwa wa dunia Itali wameikubali shingo upande hatima yao jana pale Spian ilipovunja mwiko wa miaka 88 wa kutoishinda Itali.Itali ilianza kwa kupepesuka na kaburi waliochimbiwa na Holland walipowazaba wataliana mabao 3:0 walizikwa jana na Spain. waazurri ni tofauti na ile timu iliotwaa kombe la dunia Ujerumani 2006.Waazurri walikata tiketi ya kombe hili la ulaya kwa kuilaza Ufaransa 2:0,lakini licha ya ushindi huo hawakuboresha mchezo wao.Jogoo lao Luca toni, liloongoza katika orodha ya watiaji magoli katika bundesliga, hakufua dafu mara hii.La Gazzetta dello Sport-gazeti la dimba la Itali limeandika,

"Mashabiki wa Spian waliokua wakishangiria mjini Madrid wakuiliza:Toni ulikuwa wapi ?"

Sasa mashabiki wanauliza: nini hatima ya kocha wa Itali Roberto Donadoni ?

Rais wa shirikisho la dimba la Itali, Giancarlo Abete

alikataa jana kusema iwapo Donadoni atabakia kocha wa Itali au la.

Ushindi wa Spian, jana ulitokana na kipa wao Iker Casillas

aliezima mikwaju 2 ya penalty ya Itali-wa kwanza aliouchapa De Rossi na wapili Antonio di Natale.

Vyombo vya habari vya Spian vimeshangiria ushindi wa jana kupitia mikwaju ya penalty dhidi ya mabingwa wa dunia-Itali.Yameelezea matumaini kwamba sasa watoto wa kocha mzee Luis Aragones watasonga mbele hadi finali.

Gazeti la kila siku la jiji kuu Madrid ABC lilijitokeza na kichwa hiki cha habari:

"Spian na kipa wake Iker Casillas wameishinda historia."

gazeti hapo likigusia ushindi wa kwanza kabisa wa Spian dhidi ya Itali tangu ule wa Olimpik 1920.

Mwishoni mwa wiki haikuwa Itali tu ilioaga mashindano kwa msangao wa wengi, bali hata Holland ilioanza kombe hili la Ulaya kwa vishindo.Holland iliwatimua mabingwa wa dunia Itali kwa 3:0.Halafu ikatamba mbele ya makamo-bingwa wa dunia Ufarans´a kwa 4:1.

Ulimwengu mzima ukaduawaa kwa mchezo wao wa kuhujumu moja kwa moja.Dhidi ya Urusi jumamosi, wadachi walizimwa tena na mbinu za mdachi mwenzao kocha wa Russia Guus Hiddink.

Mwenyewe Hiddink alisangaa jinsi mbinu zake zilivyoiangusha nchi yake Holland ?

"Kuwapiku holland kwa mbinu za mchezo na kwa nguvu ilikua ajabu sana.Baada ya mchezo ule nisingependa kusema mengi,kwani ilikaribia kuwa miujiza waliofanya vijana wangu."

Alisema Guus Hiddink-kocha alieiongoza korea ya kusini hadi nusu-finali ya kombe la dunia 2002.

Leo na kesho ni mapumziko katika kombe la Ulaya la mataifa.Macho lakini yanakodolewa changamoto ya jumatano hii:Ujerumani ikicheza na Uturuki.

Inatarajiwa sasa mabingwa mara 3 wa Ulaya na dunia-Ujerumani watatamba na kukata kati ya wiki hii tiketi zao za finali jumapili ijayo.Lakini, kombe hili la ulaya,haliendi hivyo.

Nani alietazamia Russia au Spian kufika hatua hii ?

Ujerumani na Uturuki ni mpambani wa aina maalumu.Waturuki kiasi cha milioni 2.5 wanaishi Ujerumani na hadi laki 1 mjini Berlin.

Kipa wa Ujerumani Jens Lehmann amekulia na waturuki na amecheza nao dimba.Anauonaje mpambano wa jumatano ?

"Natoka binafsi eneo la ruhr na nimekulia pamoja na waturuki na nimecheza sana nao dimba katika timu moja na ninawapenda.

Kwahivyo,waturiki wakiwa sehemu ya maisha yetu Ujerumani ni uzuri kuwa tunacheza nao nusu-finali."

Amesema kipa Lehmann.

Beki mshahara wa Ujerumani-maarufu wa sifa zake za kuhujumu kutoka nyuma hadi mbele asema:

"Tupanie tucheze uzuri jumatano.Kwamba utakua mchezo mgumu , hilo ni wazi.Kwani hii ni nusu-finali ya kombe la Ulaya.Juu ya hivyo, nina matumaini makubwa tutashinda."

Nje ya Kombe la Ulaya ,timu kadhaa za Afrika zilikuwa uwanjani mwishoni mwa wiki kuania tiketi zao kwa kombe la dunia na Afrika 2010.

Taifa Stars -Tanzania iliomudu sare duru ya kwanza na simba wa nyika Kamerun mjini Dar-es-salaam,iliwatembelea simba porini mwao mjini Yaounde,mwishoni mwa wiki.

Nani alinguruma ? Haikuwa Taifa Stars,kwani walizabwa mabao 2:1.

Kombe la Ulaya la mataifa likienda mapumzikoni leo na kesho, mashabiki wa Tennis ni zamu yao kupata msisimko.Mashindano mashuhuri ya ubingwa wa tennis ya wimbeledon yameanza.Swali linaloulizwa ni je, mswisi Roger Federer atawika tena na kotoroka na taji la 6 ?

Na je, upande wa wawanawake akina dada serena na Venus willaim watatamba tena ? Tusubiri kuona.

►◄