1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SREBRENICA: Kumbukumbu za mauaji ya halaiki ya Waislamu zafanyika

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjq

Jamii za wahanga wa mauaji ya halaiki ya Srebrenica huko Bosnia Herzegovina, wamehudhuria maombolezi ya kukumbuka miaka 12 ya mauaji hayo.

Kwa mara ya kwanza kumbukumbu hizo zimefanyika huku kukiwa na matumaini kwamba waliohusika katika mauaji ya Waislamu 8,000 wakiwemo wanaume na vijana, hatimaye watahukumiwa.

Mabaki ya waislamu zaidi ya 450 waliouwawa miaka 12 iliyopita huko Srebrenica, katika mauaji mabaya zaidi kuwahi kufanywa barani Ulaya tangu kumalizika kwa vita vya pili va dunia, yamezikwa hii leo.

Muongozaji mkuu wa mashtaka ya uhalifu wa kivita wa Umoja wa Mataifa, Carla Del Ponte, amehudhuria maziko hayo.