1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinbrück mgombea wa SPD kiti cha kansela

2 Oktoba 2012

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo(02.10.2012)wamejishughulisha na uteuzi wa mgombea wa kiti cha ukansela kwa chama cha SPD, siku ya muungano, pia mjadala katika baraza kuu la umoja wa mataifa kuhusu Syria.

https://p.dw.com/p/16Ien
Nordrhein-Westfalen/ Der designierte Spitzenkandidat der SPD fuer die Bundestagswahl 2013, Peer Steinbrueck, spricht am Samstag (29.09.12) in Muenster beim Parteitag der nordrhein-westfaelischen SPD. Auf der Tagesordnung des Parteitags steht unter anderem die Neuwahl des Landesvorstandes. (zu dapd-Text) Foto: Sascha Schuermann/dapd.
Peer Steinbrück ameteuliwa na SPD kuwa mgombea wa chama hichoPicha: Sascha Schuermann/dapd

Gazeti la Neue Osnabrücker Zeitung, likizungumzia kuhusu uteuzi wa Steinbrück kugombea kiti cha ukansela katika uchaguzi utakaofanyika mwakani, linaandika:

"Steinbrück jana alivuka kikwazo kingine katika njia yake kuelekea kuwa mgombea wa chama cha SPD. Kura za uongozi wa chama hicho zinajionyesha wazi. Hii ina maana , bawa la kushoto la chama hicho linaonekana kupata shauku zaidi na Steinbrück na limeendelea kumuunga mkono. Kwa upande wa bawa hilo la kushoto la SPD , pia lengo lao ni kurejea katika nguvu za uongozi wa serikali, ili kuweza kuelekeza tofauti wanazolenga za kisiasa".

Berlin/ ARCHIV: Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) und der damalige Bundesfinanzminister Peer Steinbrueck (SPD) unterhalten sich im Bundestag in Berlin auf den hinteren Plaetzen (Foto vom 27.03.09). Steinbrueck tritt als SPD-Spitzenkandidat bei der Bundestagswahl 2013 an. Dies bestaetigte die fruehere Justizministerin Brigitte Zypries am Freitag (28.09.12) auf ihrer Facebook-Seite. (zu dapd-Text) Foto: Michael Gottschalk/dapd
Steinbrück (kulia)na kansela MerkelPicha: dapd

Gazeti la Nürnberger Zeitung, likizungumzia kuhusu mada hiyo, linaandika:

"Steibrück , iwapo leo hii angekuwa farasi, ambaye hana uzoefu wa mashindano ya kimataifa, lakini amepewa uwezo wa kwenda mbio, Iwapo itawezekana kumsimamisha , hilo ni suala la kujadiliwa . Kwa upande wa ushindi hii bila shaka ni njia ambayo amekwisha pitia, kama utaangalia kwa upande wa wakati alipokuwa waziri wa fedha wa Ujerumani. Lakini wakati huo chama chake kilikuwa mshirika wa kansela wa sasa , ambapo maoni ya wapiga kura yanaonyesha kuwa bado chama chake kiko nyuma".

Mada nyingine iliyowashughulisha wahariri ni kuhusu mjadala unaoendelea katika baraza kuu la umoja wa mataifa kuhusu Syria. Mhariri wa gazeti la Märkische Oderzeitung la mjini Frankfurt anaandika:

"Umoja wa mataifa unaonyesha kwa mara nyingine tena , kuwa si chombo ambacho kinaweza kuleta suluhisho katika mizozo, kama ilivyokusudiwa, kutokana na picha ya dunia hii inavyojionyesha. Madaraka yake yamekwama, lakini hakuna ajuwae, iwapo itawezekana kuanzisha taasisi nyingine kama hii ambayo itafanyakazi vizuri zaidi. Ama iwapo hiyo itakuwa bora zaidi kuliko hii tuliyonayo".

Walid Moallem, Foreign Minister of Syria, addresses the 67th session of the United Nations General Assembly at U.N. headquarters, Monday, Oct. 1, 2012. (Foto:Jason DeCrow/AP/dapd)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Syria Walid MoallemPicha: dapd

Kuhusu mada hiyo, gazeti la Hannoversche Allgemeine Zeitung linaandika.

"Mwishoni mwa mwaka huu Ujerumani itaondoka katika baraza la usalama la umoja wa mataifa baada ya kuwapo huko kwa muda wa miaka miwili. Tathmini ya miaka hii miwili ni mbaya. Vuguvugu la mageuzi katika mataifa ya Kiarabu limekuja bila ya umoja wa mataifa kujua na kujitayarisha. Hivi leo Urusi na China zinazuwia kwa kutumia kura ya veto, uwezo wa kuwalinda raia wa Syria dhidi ya serikali yao. Haishangazi basi , kwamba wakosoaji wa umoja wa mataifa wameanza kujitokeza. Mkataba wa umoja wa mataifa unatajwa kuwa ni chombo kitakacholeta maafa makubwa kwa dunia kuhusiana na vita. Haki ya kuwa na kura ya veto inaonekana hii leo kuwa kinyume chake".

Kwa upande wa siku ya muungano wa Ujerumani, gazeti la Berliner Morgenpost linaandika:

Drei in Schwarz, Rot und Gelb gekleidete Figuren gehen am Samstag (02.10.1999) während des Bürgerfests zum Tag der deutschen Einheit am 3. Oktober durch die Wiesbadener Innenstadt. Unter dem Motto "Gemeinsam leben - gemeinsam feiern" begehen die Hessen und tausende von Gästen aus Deutschland und Europa zwei Tage lang den Geburtstag des einheitlichen deutschen Staates. Hessen hat derzeit die Präsidentschaft im Bundesrat inne und richtet damit das Fest aus. dpa/lhe (Digitale Fotografie)
Ishara ya umoja raia wamejipaka rangi ya bendera ya muunganoPicha: picture-alliance/dpa

"Helmut Kohl , ambaye katika siku hii , iwapo kuchaguliwa kwake kuwa kansela miaka 30 iliyopita kulithaminiwa , hii inaweza kuangaliwa katika kiwango kingine kisiasa, kwamba alileta muungano , na mshikamano katika bara la Ulaya , na pia katika uchumi ni kwamba , kumekuwa na umoja wa kiuchumi pia. Kisiasa , alikuwa na mtazamo wa kuwa na Ulaya ambayo ni nguzo ya amani. Kwasababu , kwa kutaka kuepuka hali ya kutoaminiana, Kohl aliona haja ya kuiunganisha nchi ya Ujerumani. Hata hivyo hatua za muungano wa Ujerumani na Ulaya bado zinaendelea ,kuwa katika hatua za mabadiliko".

Mwandishi : Sekione Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Khelef