1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier atetea mkutano wake na waziri wa kigeni wa Syria

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CuHF

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza, Frank Walter Steinmeier, ameutetea mkutano kati yake na mwenzake wa Syria,Walid la Moualem, akisema nchi hiyo ina uwezo wa kusaidia au kuvuruga amani ya Mashariki ya Kati.

Frank Walter Steinmeier amekosolewa na Marekani na Lebanon kwa kukukutana na waziri wa mashauri ya kigeni wa Syria hapo jana mjini Berlin.

Marekani inapania kuitenga Syria kwa kuwa na jukumu la kuvuruga mambo nchini Lebanon na kwa kuyadhamini makundi ya kigaidi yanayoendeleza machafuko nchini Israel.

Waziri Steinmeier ameitolea mwito Syria itumie ushawishi wake kusaidia uchaguzi wa rais nchini Lebanon na kulishawishi kundi la Hamas likomeshe mashambilizi ya maroketi dhidi ya Israel.