1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stuttgart kumsajili bingwa wa dunia Grosskreutz

5 Januari 2016

Taarifa zinasema VFB Stuttgart ya Ujerumani iko ukingoni mwa kumsajili mchezaji wa zamani wa Borussia Dortmund Kevin Grosskreutz pamoja na mshambuliaji kutoka Ukraine Artem Kravets

https://p.dw.com/p/1HY0u
Fußball DFB-Pokal 2. Runde FC St. Pauli Borussia Dortmund
Picha: picture-alliance/dpa/Daniel Bockwoldt

Pia Hannover 96 imemsajili mchezaji wa kimataifa wa Hungary Adam Szalai kwa mkopo kutoka klabu ya Bundesliga ya Hoffenheim, kwa mujibu wa taarifa kutoka klabu hiyo leo.

Wakati huo huo Manchester City inapanga kumvuta mchezaji wa kati wa Schalke 04 Leroy Sane kwa kutenga kitita cha euro milioni 55 ili kupata saini yake.

Hata hivyo meneja wa timu ya Schalke Horst Heldt amekataa kumwachia mchezaji huyo chipukizi wa timu ya taifa ya Ujerumani.

Nayo Arsenal London inasemekana imetenga kitita cha euro milioni 57 kumnyakua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang, ambaye mkataba wake na Borussia inakwenda hadi mwaka 2020.

Hizo ni baadhi tu ya taarifa katika soko la uhamisho wa wachezaji katika dirisha dogo mwezi huu wa Januari, ikiwa ni pamoja na uvumi unaoendelea kusambaa katika magazeti na vyombo vingine vya habari za michezo barani Ulaya kwa sasa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe / rtre
Mhariri: Mohammed Khelef