1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan,miaka mitatu baada ya makubaliano ya amani

Hamidou, Oumilkher9 Januari 2008

Makubaliano ya amani ya Sudan

https://p.dw.com/p/Cn4i
Rais Omar el Bashir wa SudanPicha: AP

Sudan inaadhimisha miaka mitatu hii leo tangu yalipotiwa saini makubaliano ya amani yaliyolengwa kumaliza vita vya muda mrefu kabisa vya wenyewe kwa wenyewe barani Afrika kati ya serikali ya mjini Khartoum na waasi wa zamani wa kusini mwa nchi hiyo.


Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika pakiwepo kitisho cha kuibuka tena uhasama kati ya pande mbili.Kinyume na mwaka jana,hakuna sherehe kubwa zilizoandaliwa kuadhimisha makaubaliano ya amani yaliyotiwa sain i january tisaa mwaka 2005,na kumaliza miaka 21 ya vita vilivyoghamrimu maisha ya watu wasiopungua milioni mbili.


Watu wengine kadiri milioni sita wameyapa kisogo mapigano yaliyoangamiza pia mhimili wa uchumi wa Sudan ya kusini.


Mwaka jana maandamano yaliyoitishwa Juba-mji mkuu wa kusini mwa Sudan yalikua chanzo cha malumbano kati ya rais Omar el Bashir na makamo wa kwanza wa rais Salva Kiir.


Kiir alimlaumu Bashir kwa kushindwa kutekeleza makubaliano huku Bashir akiituhumu serikali ya Kiir na kundi lake la waasi wa zamani wa SPLM kuhusika na rushwa na uongozi mbaya.


Uhusiano umevurugika tangu makubaliano tete ya amani yalipokumbwa na mzozo mbaya kabisa October 13 iliyopita,pale mawaziri wa kusini mwa Sudna walipojitoa katika serikali ya umoja wa taifa wakilalamika dhidi ya kile walichokiita " kuzoroteshwa makaubaliano ya amani ya CPA na maafisa wa kaskazini mwa Sudan."


Mzozo huo ulimalizika december iliyopita pale mawaziri waliojiunga na serikali walipobuni ratiba ya jinsi ya kutia njiani makubaliano hayo.


Jana na kuambatana na makubaliano hayo,vikosi vya kaskazini vikayahama hatimae maeneo tajiri kwa mafuta kusini mwa Sudan-baada ya kuchelewa kuyahama maeneo hayo kama ilivyopangwa december 31 iliyopita.


Kiir binafsi ameanza upya kujitokeza katika majukwaa ya kisiasa mjini Khartoum na katika vyombo vya habari.


Bashir amesisitiza kwa mara nyengine tena vita havitashuhudiwa tena nchini Sudan ,licha ya mwito uliotolewa November iliyopita na wanamgambo wa chama cha national Congress kujiandaa kwaajili ya mapigano.


"Vita havina faida yoyote isipokua kumwaga damu na havileti chochote isipokua kusababisha watoto kua yatima na wakinamama kua wajane."Amesema hayo Bashir katika hotuba yake hapo jana.


Mada tete zilizosalia ni kuhusu kanuni za enbeo tajiri kwa mafuta la Abyei,ambalo kila upande unadai kua ni sehemu ya ardhi yake-mahala unakopangwa kuchorwa mpaka kati ya kaskazini na kusini.


Wanamgambo wenye asili ya kiarabu na kuungwa mkono na serikali ya mjini Khartoum ,wanaendelea kuwahujumu wanajeshi wa SPLM katika maeneo ya kusini na mapigano ya hivi karibuni yamegharimu maisha ya watu dazeni kadhaa.


Kuambatana na makubaliano ya CPA,uchaguzi umepangwa kuitishwa mwaka 2009 na kura ya maoni itakayofuatia miaka miwili baadae,itawaruhusu wakaazi wa kusini kutamka kama wanataka kuendelea kuishi na wenzao wa kaskazini au wan ataka kua huru.

►◄