1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SUVA: Serikali ya mptio yateuliwa Fiji

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcU
Rais George W. Busha akizungumza na Rais Vackav Klaus wa Jamhuri ya Czech mjini Prague tarehe 5 mwezi wa Juni 2007.
Rais George W. Busha akizungumza na Rais Vackav Klaus wa Jamhuri ya Czech mjini Prague tarehe 5 mwezi wa Juni 2007.Picha: AP

Kiongozi wa kijeshi nchini Fiji, Frank Bainimarama ameteua serikali ya mpito. Wiki iliyopita, Bainimarama aliapishwa kuwa waziri mkuu wa Fiji, mwezi mmoja tangu alipoipindua serikali bila umwagaji damu.

Viongozi waliokuwa katika serikali ya zamani, makamanda wa jeshi na maofisa wa ngazi za juu wamejumulishwa katika baraza la mawaziri la serikali ya mpito.

Frank Bainimarama amesema serikali yake itafanya juhudi kurejesha demokrasia nchini Fiji, lakini mpaka sasa bado hajatangaza tarehe ya uchaguzi mpya.