1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDEY:Bush asema hatoitupa mkono Iraq

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSc

Rais George Bush wa Marekani amewasili Australia kwa ajili ya mkutano wa kilele wa wakauu wa nchi za Asia na Pacific ambako amekuwa na mazungumzo pembezoni mwa mkutano huo na viongozi wengine.

Rais Bush amewasili mjini Sydey akitokea Iraq alikofanya ziara ya ghafla ambako alimuhakikishia Waziri Mkuu wa Iraq Nuri Al Maliki ya kwamba Marekani haitawatelekeza watu wa Iraq.

Wakati huo huo Mahakama Kuu ya Iraq imeridhia hukumu ya kifo aliyopewa Waziri wa Ulinzi katika serikali ya Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein, Ali Hassan al Majid maarufu kama Chemical Ali.

Chemical Ali ambaye ni binamu yake Saddam Hussein na watu wengine wawili walihukumiwa kunyongwa mwezi June baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya mauaji ya halaiki na makosa ya uhalifu wa kivita.

Wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya maelfu ya wakurdi katika harakati za kuwaangamiza za mwaka 1988 zilizoitwa Anfal.

Kwa mujibu wa sheria za Iraq wanatarajiwa kunyongwa ndani ya kipindi cha siku 30.