1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY:Uchunguzi waendelea Australia

6 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlE

Polisi nchini Australia wamewahoji madaktari wengine watano na kufanya msako katika hospitali mbili ili kutafuta watu wanaoaminika kuhusika na jaribio la shambulio la wiki jana nchini Uingereza.Hatua hiyo inachukuliwa baada ya daktari mmoja aliye na asili ya Kihindi kukamatwa mwanzoni mwa wiki hii katika jimbo la mashariki la Queensland.Yapata madaktari wengine 5 walizuiliwa nchini Uingereza kuhusiana na jaribio hilo la shambulio la bomu katika miji ya Glasgow na London.

Polisi walisaka miji ya Perth na Kalgoorlie magharibi mwa Australia na kuwahoji kwa muda mfupi madaktari 4 walio na asili ya Kihindi waliofanyakazi awali nchini Uingereza. Mick Keelty ni Kamishna wa Polisi nchini Australia

''Tunachojaribu kufanya ni kujua ni kina nani waliohusika .Hii haimaanishi kuwa tunaowahoji wana hatia ila tunajaribu kujua iwapo wanahusika na vitendo vya uhalifu vyo London na Glasgow.Shughuli zetu hapa zinashirikiana na zile za uchunguzi uanofanyika nchini Uingereza ''

Misako hiyo na mahojiano inatokea siku moja baada ya maafisa wa huduma za afya katika eneo la magharibi mwa Australia kudai kwamba madaktari wawili wanaozuiliwa na polisi wa Uingereza walijaribu kutafuta kazi nchini Australia bila kufanikiwa.