1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria na Iran zataka kuimarisha uhusiano wao

Prema Martin25 Februari 2010

Hii leo Rais wa Syria Bashar al-Assad na rais mwenzake wa Iran Mahmoud Ahmedinejad wamepuza waziwazi jitahada za Marekani kutaka kuleta mtengano kati ya washirika hao wawili katika Mashariki ya kati.

https://p.dw.com/p/MBAa
Syrian President Bashar Assad, right, laughs during a press conference with his Iranian counterpart Mahmoud Ahmadinejad, left, in Damascus, Syria, Thursday, Feb. 25, 2010. The United States should pack up and leave the Middle East and stay out of regional affairs, Iran's president said Thursday during a visit to Damascus that follows a string of U.S. efforts to break up Syria's 30-year alliance with Tehran. (AP Photo/Bassem Tellawi)
Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad(kushoto) na Rais Bashar al-Assad wa Syria.Picha: AP

Rais Bashar al-Assad amesema kuwa ameshtushwa na wito wa Marekani kuitaka Syria ijiweke mbali na Iran na hali inazungumzia masuala ya utulivu na amani katika Mashariki ya Kati. "Ipo haja ya kuimarisha zaidi uhusiano, ikiwa kweli lengo ni kuleta utulivu. Hatutaki kufunzwa na wengine kuhusu eneo letu na historia yetu aliongezea al-Assad alipozungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanywa pamoja na Rais Ahmedinejad mjini Damascus.

Nae Ahmedinejad aliekwenda Damascus mapema leo hii, alisisitiza kuwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya Kiislamu ni imara. Huo ni uhusiano wa kindugu,wa dhati na wa daima - hakuna kitakachoweza kuharibu uhusiano huo. Enzi ya Marekani kutoa amri kwa mataifa mengine imemalizika aliongezea Ahmedinejad.

Hiyo jana, serikali ya Rais Barack Obama ilisema kuwa wakati ikijaribu kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya Marekani na Syria, vile vile imekuwa ikiishinikiza Damascus ijitenge na Iran na iache kuwapatia silaha Hezbollah. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton alieleza kinagaubaga kuhusu jitahada za kutaka kuzitenganisha Damascus na Tehran. Amesema, mwanadiplomasia wa Marekani wa ngazi ya juu William Burns alizungumza kwa urefu na kina alipokwenda Syria juma lililopita. Syria inashinikizwa kujitenga na Iran inayosababisha wasiwasi Mashariki ya Kati na hata Marekani aliongezea waziri Clinton.

U. S. Secretary of State Hillary Rodham Clinton, seen during a press, after holding talks with Prime Minister and Foreign Minister of Qatar Sheikh Hamad bin Jassim bin Jabor Al Thani, in Doha the capital of the State of Qatar, Sunday, Feb. 14, 2010. Clinton arrived Sunday in Qatar, where she is holding talks with top government leaders and speaking at the U.S.-Islamic World Forum. (AP Photo/Maneesh Bakshi)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Hillary Clinton.Picha: AP

Wakati huo huo, Washington ikipigia debe mito ya kuiwekea Iran vikwazo vipya kuhusiana na mradi wake wa nyuklia, Rais wa Syria ametetea haki ya Iran kuendelea kurutubisha madini ya Uranium. Amesema, kulizuia taifa huru, haki ya kurutubisha madini ni sawa na kuwepo utaratibu wa ukoloni mambo leo katika kanda hiyo.

Hapo awali Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Walid Muallem alisema Damascus imetia nia kuileta Iran pamoja na kambi ya Magharibi kwa majadiliano ya dhati kuhusu mradi huo wa nyuklia. Nchi za Magharibi zinahofia kuwa Iran iliyoanza kurutubisha uranium kwa kiwango cha juu mapema mwezi huu, inataka kutengeneza silaha za nyuklia kwa siri. Madai hayo yanakanushwa vikali na serikali ya Iran.

Syria na Iran zinatuhumiwa na Marekani kutoa msaada kwa makundi yenye misimamo mikali kuelekea Israel, hasa kundi la Kishia la Hezbollah nchini Lebanon na chama cha Kipalestina Hamas kinachotawala Ukanda wa Gaza.

Mwandishi:P.Martin/AFPE

Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed