1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yamlaumu Ban Ki- Moon kwa kupendelea

29 Aprili 2012

Syria imemlaumu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki- Moon, kuwa maoni yake yaliyoituhumu serikali ya nchi hiyo kuvuruga mpango wa usitishaji mapigano kuwa ni ya kupendelea.

https://p.dw.com/p/14mdS
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki MoonPicha: Reuters

Siku ya Ijumaa Moon aliwaambia waandishi wa habari kuwa vitendo vya mauawaji vinavyofanywa na serikali ya Assad havivumiliki na kuitaka nchi hivyo kutii makubaliano ya mpango wa usitishaji mapigano. Kauli hiyo aliitoa muda mfupi baada ya kufanyika kwa mashambulizi ya mabomu ambayo yaliuwa raia 10.

Bani na Annan wote walizilaumu pande zote mbili lakini waliitaja serikali kuwa ndiyo mhusika mkuu. Tahariri ya Gazeti la Shirika la Habari la nchi hiyo siku iliyofuata ilisema kuwa Moon ameshindwa kuonesha mabaya yanayofanywa na upinzani na badala yake ameelemea upande wa seriklia pekee.

Hofu ya mataifa juu ya tuhuma za Syria

Tuhuma hizo za Syria dhidi ya Moon zimezusha hofu kuwa huenda Rais Bashar al-Assad anajaribu kucheza na muda ili kukwepa kutimiza makubaliano ya usitishaji wa mapigano jambo ambalo linaweza kumsababisha akatolewa kwa nguvu madarakani.

Rais wa Syria Bashar al-Assad
Rais wa Syria Bashar al-AssadPicha: Reuters

Chini ya mapango wa usitishaji mapigano uliopendekezwa na Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Koffi Annan, waangalizi wapatao 300 wanatakiwa kwenda Syria kusimamia utekelezaji wake na kufanya mazungumzo na pande mbili yaani serikali na upinzani kuhusu mustakabali wa taifa hilo hapo siku za usoni.

Mkuu wa kikosi cha waangalizi Meja Jenerali Robert Mood anatarajiwa kuwasili mjini Damascus leo ili kuongoza kazi hiyo. Mpango huo wa Annan uliokuwa ukamilike Aprili 12 , umekiukwa kwa kiasi kikubwa. Utawala wa Assad umeendelea kuwazishambulia ngome za upinzani huku waasi nao wakivilenga vikosi vya serikali kwa kuvirushia mabomu barabrani pamoja na mashambulizi ya kushtukiza.

Shaka ya kiusalama bado yatanda

Katika kile kinachoonekana kuwa ni kushindwa kwa utawala wa Syria kutii makubaliano, nchini hiyo dhadi sasa haijaondoa silaha zake nzito na vikosi vyote katika maeneo yanayokaliwa na raia.

Moja ya miripuko katika mji mkuu wa Syria, Damascus
Moja ya miripuko katika mji mkuu wa Syria, DamascusPicha: Reuters

Nchini Syria kwenyewe mapambano yameendelea ambapo viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo Damascus vilishambuliwa. Wanaharakati nchini humo wanasema kuwa vikosi vya serikali vimefanya mashambulizi katika pwani ya bahari lilipo kasri la Assad dhidi ya watu waliokuwa na silaha ambao waliosemekana kuwa magaidi.

Serikali ilisema kuwa mashambulizi hayo yamefanywa na magaidi. Mashambulizi hayo pia yalilaaniwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Koffi Annan na ambaye alitaka kupelekwa kwa waangalizi 300 haraka nchini humo ili kusimamia hali ya mambo.

Mwandishi: Stumai George/AP
Mhariri: Mohammed Khelef