1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yatumia manowari kupambana na wapinzani

Martin,Prema/ZPR15 Agosti 2011

Nchini Syria, serikali ya Rais Bashar al-Assad inazaidi kutumia silaha kubwa, dhidi ya waandamanaji wanaodai demokrasia.

https://p.dw.com/p/RfzM
In this image taken from video made available Sunday Aug. 14, 2011, by Shaam News Network (SHAMSNN), in which they purport to show armoured vehicles as they take up positions along the water front of Latakia, Syria. The intense operation in Latakia, a key port city once known as a summer tourist draw, is part of a brutal government crackdown on several Syrian cities meant to root out protesters demanding the ousting of President Bashar Assad. (AP Photo / SHAMSNN) EDITORIAL USE ONLY - THE ASSOCIATED PRESS HAS NO WAY OF INDEPENDENTLY VERIFYING THE CONTENT, LOCATION OR DATE OF THIS VIDEO IMAGE.
Mji wa bandari Latakia, SyriaPicha: AP Photo / SHAMSNN

Kwa mujibu wa ripoti za mashahidi, mbali na vifaru na majeshi ya nchi kavu, sasa manowari zinatumiwa kushambulia maeneo yenye wakaazi wengi katika mji wa bandari wa Latakia.

Wanaharakati wa haki za binadamu wamesema, idadi kadhaa ya raia waliuawa katika mashambulio ya hapo jana. Ripoti za vyombo vya habari zinasema, kati ya watu 19 na 26 wameuawa. Wapinzani wa Assad wameamua kuendelea na maandamano yao, licha ya Latakia na miji mingine ya Syria kushambuliwa na majeshi ya serikali.