1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano kuhusu uhamiaji waibua taharuki Ujerumani

Josephat Charo
15 Juni 2018

Taharuki ya muda mfupi ilitanda (15.06.2018) Ujerumani wakati vyombo kadhaa vya habari viliponasa katika mtego wa taarifa feki ya tashtiti iliyodai kwamba serikali ya mseto ya Ujerumani ilikuwa imesambaratika.

https://p.dw.com/p/2zdhx
Berlin, Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) spricht mit Horst Seehofer (CSU)
Horst Seehofer, kushoto, na kansela Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa/M.Kappeler

Taarifa isiyo sahihi kwamba waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Horst Seehofer, angeufikisha mwisho ushirika wa miaka saba kati ya chama chake cha jimbo la Bavaria cha Christian Social Union, CSU, na chama cha kansela Merkel cha Christian Democratic Union, CDU, zimeelezwa kuwa kama bomu lililolipuka na akaunti hiyo ya twitter iliyothibitishwa.

Wakati akipokea taarifa mpya kuhusu kadhia hiyo, msemaji wa Merkel, Steffen Seibert, alifaulu kukanusha madai hayo, lakini sio kabla kuonekana kama habari zilizochipuka kwenye mtandao wa gazeti maarufu la Bild na vyombo vingine vya habari. Mwanachama wa uongozi wa chama cha CSU, Hans Michelbach, alifafanua kwa haraka kuwa madai hayo yalikuwa taarifa ya uongo iliyotokea kwa mwandishi wa jarida la tashtiti la Titanic.

Taarifa hiyo ilidai kuwa Seehofer baada ya siku kadhaa za malumbano na Merkel, alikuwa ametangaza kwa mujibu wa barau pepe ya ndani, kuufikisha mwisho ushirikiano na chama cha CDU.

Serikali ya mseto ya Ujerumani inakabiliwa na mgogoro kwa sababu ya mvutano kuhusu uhamiaji. Hali ya kutoelewana inayoendelea kuzidi kati ya kansela Merkel na waziri Seehofer kuhusu sera ya uhamiaji inatishia kusababisha mpasuko katika vyama vya kihafidhina vya Christian Democratic Union, CDU na Christian Social Union, CSU, ambavyo vinatwala pamoja na chama cha Social Democaratic, SPD.

Deutschland 70 Jahre Soziale Marktwirtschaft Angela Merkel
Kansela Angela MerkelPicha: Reuters/M. Tantussi

Mzizi wa fitina ni suala la ikiwa wakimbizi fulani wanatakiwa kukataliwa katika mpaka wa Ujerumani. Chama cha CSU, kinataka hivyo, lakini kansela Merkel anapinga na anategemea suluhisho la Ulaya, kama ulivyo msimamo wa chama cha SPD.

Merkel ashikilia msimamo wake

Akizungumzia mvutano huo mwenyekiti wa chama kinachowapendelea wafanyabiashra cha Free Democratic, Christian Lindner, alisema, "Tunataka Ujerumani isimamie suluhisho la Ulaya katika suala hili. Hatutatki kuifunga nchi yetu, hatutaki vizuizi virejee Ulaya kupitia upekuzi wa mipakani. Cha msingi ni ulinzi, udhibiti wa mpaka wa nchi, na mfumo wa haki wa kugawana wahamiaji, lakini hakuna anayejihusisha na hili Ulaya. Kila mtu anasema Wajerumani wanaubeba mzigo wote, na hapa bunge la Ujerumani lazima sasa lipitishe uamuzi."

Kansela Merkel bado anashikilia msimamo wake wa kupinga wazo la kuwazuia baadhi ya wakimbizi katika mpaka wa Ujerumani, kama wanavyotaka washirika wake serikalini. Msemaji wa Merkel, Steffen Seibert ameonya hatua hiyo huenda ikaudhoofisha Umoja wa Ulaya.

Katika siku za hivi karibuni ghadhabu ndani ya serikali imeendelea kushuhudiwa kuhusu suala hilo na mzozo huo umeibua maswali kuhusu mustakahbali wa Merkel, huku vyama vya kizalendo vilivyo madarakani kwingineko Ulaya vikikaza skurubu na kumbana Merkel kwa msimamo wake wa kuwakaribisha wahamiaji.

Wanachama wengine wa serikali ya Merkel leo walitoa kauli za kulaumiana huku mwenyekiti wa chama cha SPD, Andreas Nahles, akikilaumu chama cha CSU kwa msimamo wake kuhusu wahamiaji. "Suluhisho pekee haliwezekani wala haliingia akilini. Na ndio maana kwa mtizamo wangu, tabia ya chama cha CSU haikubaliki."

Nahles alisema chama chake kinauunga mkono wito wa Merkel wa makubaliano mapana ya Ulaya kuhusu jinsi ya kulitafutia ufumbuzi suala la uhamiaji usio halali.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macro, alisema anamuunga mkono kansel Merkel katika msimamo wake.

Mwandishi: Josephat Charo/ape/afpe

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman