1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taliban bado ni shupavu

Mohamed Dahman18 Desemba 2007

Kufuatia miaka sita ya vita,maelfu ya watu kupoteza maisha yao na kutumika kwa mabilioni ya dola kundi la Taliban linaendelea kubakia kuwa kikosi jasiri kisichopaswa kubezwa.

https://p.dw.com/p/Cd23
Mullah Mohamed Omar kiongozi wa Taliban ambaye bado anasakwa na vikosi vya Marekani nchini Afghanistan.Picha: AP

Wakati theluji ya kwanza ikidondoka milimani mwaka mwengine umemalizika bila ya kuwepo kwa matumaini ya wazi ya kuleta amani katika nchi ilioathiriwa na vita ya Afghanistan ambayo kwa kwa zaidi ya miongo mitatu imekuwa kwenye machafuko.

Mwaka wa 2007 ulikuwa na umwagaji damu mkubwa zaidi tokea uvamizi ulioongozwa na Marekani kuungusha utawala wa Taliban kwa kudhamini kundi la Al Qaeda na Osama bin Laden aliepanga mikakati ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 dhidi ya miji ya Marekani.

Zaidi ya watu 6,000 wengi wao wakiwa ni waasi lakini pia wakiwemo mamia ya wanajeshi wa Kiafghan na wale wa kimataifa na takriban raia 1,000 wameuwawa kwenye umwagaji damu huo. Idadi ya vifo kwa mwaka wa 2007 ilikuwa juu zaidi kwa asilimia 50 kuliko ilivyokuwa mwaka 2006 na ulikuwa pia ni mwaka wa umwagaji mkubwa wa damu kwa vikosi vya Marekani ambapo zaidi ya wanajeshi wake 100 wameuwawa.

Kumetokea zaidi ya mashambulizi 120 ya kujitolea muhanga mwaka huo mbinu ambayo ilikuwa haijulikani nchini Afganistan kabla ya mwaka 2003.Shambulio baya kabisa lilitokea kwenye jimbo ambalo kwa wastani ni tulivu la Baghlan hapo mwezi wa Novemba ambapo zaidi ya watu 80 wameuwawa wakiwemo wa wabunge sita wa serikali tete ya nchi hiyo.

Wanamgambo wa Taliban pia wameuwa wanajeshi kadhaa wa Kiafghan na wa kigeni katika mashambulizi ya mabomu yanayotegwa kandoni mwa barabara wakitumia mbinu za kuwaigiza waasi nchini Iraq.

Waasi pia wamehasirika sana kwa kuwapoteza makamanda wao waandamizi 80 na idadi ya makada isiojulikana inaokadiriwa kufkia maelfu.Hapo mwezi wa May kamanda mwandamizi wa kijeshi Mullah Dadullah aliuwawa katika operesheni ilioongozwa na Marekani kwenye jimbo la vurugu la kusini la Helmand.

Wanagambo huo wa Taliban inaaminikwa kwamba wamekuwa wakijiamarsiha kwa kuwaorodhesha makuruta wapa kutoka makambi ya wakambizi wa Afghanistan na kwenye maeneo tete nchini Pakistan na maeneo ya kabila la Wapashtun karibu na mpaka.Mavuno ya kasumba inayotumiwa kutengeneza madawa ya kulevya yamefikia kiwango cha kutisha na inakadiriwa kwamba hugharamia sehemu kubwa sana ya gharama za kuendesha vita za kundi hilo.

Kwa mujibu wa Qasim Akhgar mwandishi wa Afghanistan na mchambuzi wa kisiasa ulikuwa ni mwaka wa propaganda kwa Taliban ambao wameteka wilaya kadhaa kusini na mashariki mwa nchi hiyo na kuanza kutumia mbinu mpya ya kuteka nyara.

Kwa kubadilishana na mwandishi wa habari wa Italia Taliban ilifanikisha kuachiliwa huru kwa wenzao watano waliokuwa gerezani.Utekaji nyara zaidi ulifuatia ambapo Taliban iliilazimisha serikali ya Korea Kusini kufanya nayo mazungumzo ya ana kwa ana kwa ajili ya kauchiliwa kwa raia wake 23 waliokuwa wakiwashikilia mateka.

Pia kumekuwepo na ushahidi wa kuingizwa nchini humo kwa makundi ya wapiganaji na shehena ya silaha kupitia mpakani kwa ajili ya Taliban.

Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama kinachhongozwa na NATO ambacho kina wanajeshi 41,000 kutoka nchi 38 pia kimegawika hadharani juu ya kutuma vikosi zaidi na zana ili kutanuwa shughuli zao.

Vikosi vya Marekani,Uingereza na Canada vinapambana na uasi katika mikoa ya kusini na mashariki karibu kila siku lakini nchi nyengine wanachama wa NATO kama vile Ujerumani,Ufaransa na Uhispania zinagoma kupeleka wanajeshi wao katika majimbo yenye mapigano.