1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TALLIN:Sanamu ya kisoviet kurejeshwa nchini Estonia

29 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC5x

Serikali ya Estonia imesema kuwa sanamu inayokumbusha enzi za kisoviet iliyoondolewa na kusababisha mgogoro nchini humo itarejeshwa mapema mwezi ujao na kuwekwa kwenye makaburi ya mashujaa wa vita kuu vya pili.

Wazalendo wa Estonia wanapinga sanamu hiyo ya askari kwa sababu inawakumbusha enzi ambapo nchi yao ilikaliwa na utawala wa kisoviet.Lakini waEstonia wenye nasaba ya kirusi wanasema sanamu hiyo ni ukumbusho wa askari waliojitoa mhanga katika vita vya kupambana na majeshi ya mafashisti wakati wa vita kuu vya pili.