Tamaduni mbalimbali nchini Ujerumani ?
17 Oktoba 2010POTSDAM:
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema juhudi za kuwaleta pamoja watu wa tamaduni mbalimbali nchini Ujerumani zimeshindikana kabisa.
Kansela Merkel aliyasema hayo mjini Potsdam kwenye mkutano wa tawi la vijana la chama chake cha kihafidhina CDU . Ameeleza kuwa itakuwa vigumu kuyafuta makosa yaliyofanyika kwa muda wa miaka mingi iliyopita.Kiongozi huyo wa Ujerumani pia ametahadharisha dhidi ya kuhimiza uhamiaji bila ya kufanya matayarisho ya kutosha.Ameeleza kuwa haipasi kusalimu amri mbele ya mwito wa kuhimiza uhamiaji wa kiwango kikubwa bila ya kwanza kufanya kila linalopasa kujenga uwezo wa wananchi wazaliwa na kuwapa fursa.
Kansela Merkel pia amesisitiza kwamba wahamiaji wanapaswa kujijumuisha na jamii na wajifunze lugha ya Kijerumani,lakini pia amesema anatambua umuhimu wa wahamiaji katika maendeleo ya uchumi wa Ujerumani.