1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania kupeleka kikosi Dafur

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CPlS

Tanzania itachangia wanajeshi 800 katika kikosi mchanganyiko cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuleta utulivu na kukomesha mauaji ya raia katika jimbo la Dafur nchini Sudan.

Waziri wa Ulinzi Juma Kapuya amesema wanajeshi wake watakaowekwa Dafur hapo mwezi wa Machi hawatohusika na mapambano wakati wakipiga doria katika jimbo hilo ambapo tayari wanajeshi wa kulinda amani wamekuwa wakishambuliwa na kuuwawa.

Kwa mujibu wa Kapuya wana baraka zote za serikali ya Sudan ambayo imeiomba Tanzania kuchangia kwenye kikosi cha kimataifa cha kulinda amani kuleta utulivu Dafur.