1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

26 Aprili 2010

Watanzania leo, April 26, wanaadhimisha miaka 46 tangu kuundwa Muungano wa zilizokuwa dola huru za Tanganyika na Visiwa vya Zanzibar, hivyo kuzaliwa kwa taifa jipya la Tanzania.

https://p.dw.com/p/N75x
Jiji la Dar es Salaam,TanzaniaPicha: DW /Maya Dreyer

Tokeo hilo lilifanyika wakati wa kusisimua katika siasa za Bara la Afrika, punde baada ya nchi nyingi za Afrika kupata uhuru, na miezi mitatu tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.

Mmoja kati ya mashahidi wa kuzaliwa Muungano huo ni Job Lusinde, waziri katika serikali ya Tanganyika punde baada ya uhuru mwaka 1961, na pia aliitumikia serikali ya Muungano.

Sansibar Stonetown
Mji Mkongwe wa Zanzibar,TanzaniaPicha: DW /Maya Dreyer

Othman Miraji amezungumza na Bw Job Lusinde huko kwake Dodoma na kwanza kumuuliza nini kilichowachochea waasisi wa Muungano huo, marais wa Tanganyika na Zanzibar, Julius Nyerere na Abeid Karume kuja na wazo hilo:

Mahojiano: Othman Miraji/Job Lusinde

Mpitiaji:Abdul-Rahman