1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Waziri Membe azungumzia kuhusu uraia wa nchi mbili

27 Agosti 2013

Serikali ya Tanzania iko mbioni kuwaruhusu wananchi wake kuwa na uraia wa nchi mbili baada ya kubaini kuwa idadi kubwa ya raia walioko nchi za ng'ambo wanakosa fursa za kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.

https://p.dw.com/p/19XNN
Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa kimataifa
Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa kimataifaPicha: Getty Images

Serikali ya Tanzania iko mbioni kuwaruhusu wananchi wake kuwa na uraia wa nchi mbili baada ya kubaini kuwa idadi kubwa ya raia walioko nchi za ng'ambo wanakosa fursa za kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.

Katika kufanikisha shabaha yake hiyo, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe amepeleka pendekezo rasmi kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akitaka akitaka suala la uraia wa nchi mbili kitambulike kwenye katiba ijayo. Mwenzetu George Njogopa alikutana na Waziri Membe jijini Dar es saalam na kumuuliza sababu za kupekeka mapendekezo hayo katika tume ya mabadiliko ya katiba.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Mohammed Khelef