1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yatuhumiwa kusuasua kutekeleza malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mohamed Dahman1 Novemba 2008

Tanzania yatuhumiwa kwa kutojifunga kwa dhati kutimiza malengo ya Jumuiya ya Afrika mashariki kwa hoja kwamba watu wake hawako tayari kwa muungano wa kuifanya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa shirikisho la kisiasa 2015.

https://p.dw.com/p/FlZE

Hoja zinazotolewa ni kwamba
miundo yake ya kisiasa na kiuchumi haiwezi kukidhi mahitaji ya muungano huo ambayo yanataka kuondolewa kwa vikwazo vyote vya biashara, kuruhusu usafirishaji huru wa bidhaa na utowaji wa huduma.

Mohamed Dahman na kusua sua kwa Tanzania katika kufanikisha malengo ya jumuiya hiyo.

_________________________________________________

Walikuwa ni raia sita wa Kenya wanaofanya kazi katika chombo kikubwa kabisa cha habari afrika mashariki na kati ambayo ni kampuni ya Nation Media Group na walikuwa wakitakiwa kuonyesha thamani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuruhusiwa kutumia ujuzi wao katika nchi jirani ya Tanzania.Huo ulikuwa ni mwaka 2005.

Kwa hatua kubwa msimamo huo ulitiwa moyo wakati huo na mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliosainiwa na hapo mwezi wa Novemba mwaka 1999 na Rais Daniel Arap Moi wa Kenya,Benjamin Mkapa wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda.

Kwa muijibu wa mkataba huo kipengele kikuu ilikuwa ni kuruhusu nyendo huru za kufanya kazi kati ya nchi hizo tatu.

Lakini mabalozi hao sita wa Afrika Mashariki walikuja kufungishwa virago kwa idhara na kuonyesha hatari sugu ya kuwaamini wanasiasa wa Kiafrika.

Miaka mitatu baadae mwishoni mwa mwezi wa Septemba mwaka huu nchini Burundi katika duru ya tatu ya mazungumzo ya itifaki ya soko la pamoja la jumuiya hiyo ikiwa imetanuka kwa kuzijumuisha Burundi na Rwanda serikali ya Tanzania kutokana na shinikizo ilikubali kuondowa upinzani wake kwa raia kutoka nchi nyengine wanachama kuwa na haki ya ukaazi katika nchi za jumuiya kwa dhamira ya shughuli za kiuchumi au ajira.

Wanachama wapya katika jumuiya hiyo Burundi na Rwanda zilijiunga na jumuiya hiyo hapo mwaka 2007 na kuifanya jumuiya hiyo kuwa na nguvu barani Afrika ikiwa ni idadi ya watu milioni 120 na pato la uzalishaji wa jumla wa ndani ya nchi la dola bilioni 41.

Cha kutiliwa maanani ni kwamba jumuiya hiyo imekuwa ikifanya kazi kama umoja wa forodha tokea mwaka 2005 ukiruhusu bidhaa kutoka Uganda na Tanzania kuingia Kenya bila ya ushuru wakati zile za Kenya zinazoingia nchini humo zinatozwa uhuru hadi hapo mwaka 2010 kwa hoja ya kuziwezesha nchi nyengine wanachama wa jumuiya hiyo kupiga hatua ya maendeleo ya kiuchumi kulingana na ile ya Kenya.

Watafiti wanaona kwamba tishio halisi linalokabili mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni ishara zinazotolewa na Tanzania mfano ikiwa ni kauli ya naibu waziri wa ushirikiano wa jumuiya ya Afrika Mashariki Mohamed Aboud katika mahojiano na gazeti mashuhuri la Citizen kwamba kimsingi Tanzania haipingi wageni kufanya kazi nchini humo kwani ina uhaba wa madaktari,wahandisi na wataalamu wengine lakini baraza lao la mwaziri inabidi litaarifiwe kwanza juu ya matokeo ya mkutano wa Burundi wa mwezi wa Septemba.

Waziri mwenyewe wa wizara hiyo Diodorus Kamala aliwahi kusema huko nyuma kwamba wasiokuwa raia nchini humo wasiruhusiwe kununuwa ardhi na hata katika mkutano wa Burundi Tanzania ilipinga kifungu katika itifaki kwa raia wa nchi wanachama kuwa na haki ya kumiliki ardhi.

Itakumbukwa kwamba Rais Yoweri Museveni wa Uganda hapo mwaka jana alikuwa na ujumbe mkali kwa Tanzania kwa kusema kwamba wasonge mbele na malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki aidha kwa kuihusisha au kutoihusisha Tanzania.