1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TBILISI: Watu watatu wauwawa kwenye mripuko wa gesi

27 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyi

Watu watatu wameuwawa kwenye mripuko kwenye kituo cha gesi ya oxygen katika mji mkuu wa Georgia, Tbilisi. Watu wengine wawili wamejeruhiwa vibaya katika mripuko huo uliokiharibu kabisa kituo hicho.

Msemaji wa idara inayohusika na shughuli za uokozi amesema inahofiwa huenda maiti mbili au tatu zikawa zimefunikwa chini ya vifusi. Mripuko huo umeelezwa kuwa ajali.