1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TBILISI:Bunge laidhinisha hali ya hatari

9 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBKN

Bunge nchini Georgia linaidhinisha hatua ya Rais Mikheil Saakashvili ya kutangaza hali ya hatari itakayodumu hadi Novemba 22.Wabunge wote 149 waliohudhuria kikao cha bunge waliidhinisha agizo hilo lililotolewa siku ya Jumatano baada ya ghasia kuzuka mjini Tbilisi kati ya polisi na waandamanaji.Hatua hiyo inalazimu vituo vya televisheni kuendelea kufungwa kwa yapata siku 15. Batu Kutelija ni naibu Waziri wa Ulinzi wa Georgia

''Kwanza kabisa nataka kusema kuwa hali ya hatari ilitangazwa kulingana na sheria na kanuni za Georgia na vikwazo vyote vilivyowekwa vinaambatana na sheria za nchi.Kwahiyo sidhani hilo litasababisha rais na serikali ya Georgia kutoaminika hasa kwavile alitakiwa kutangaza uchaguzi wa mapema wa rais.''

Wabunge wa upinzani walisusia kikao hicho.

Kiongozi wa Georgia Mikheil Saakashvili ametangaza kufanyika kwa uchaguzi wa mapema na kuahidi kubatilisha sheria ya hali ya hatari haraka iwezekanavyo.Polisi bado wanaendelea kushika doria mjini Tbilisi kufuatia ghasia kuzuka kati ya majeshi ya usalama na waandamanaji wanaopinga serikali.Bwana Saakashvili anatangaza uchaguzi kufanyika tarehe 5 mwezi Januari.Uchaguzi huo wa rais ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka ujao. Bwana Saakashvili alikabiliwa na shinikizo kutoka jamii ya kimataifa baada ya kutangaza hali ya hatari ya siku 15 baada ya ghasia kutokea siku ya jumatano.