1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Uingereza iashirie nia njema

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBV

Iran imekanusha kuwa iliwatesa wanamaji 15 wa Uingereza waliowazuia kwa takriban majuma mawili. Siku ya Alkhamisi kwenye mkutano na waandishi wa habari,wanamaji hao walieleza jinsi walivyovuliwa nguo na kuzibwa macho.Wamesema,wakati wote walitenganishwa na kuwekwa peke yao.Vile vile wamesema,hapo mwanzoni,wakiwa wamefumbwa macho, waliwekwa dhidi ya ukuta kama kutayarishwa kupigwa risasi.Kwa upande mwingine,Teheran inasema,matamshi ya wanamaji hao yametolewa chini ya shinikizo la serikali.Wakati huo huo balozi wa Iran mjini London amesema,kufuatia kuachiliwa huru wanamaji hao 15,Uingereza inapaswa kutoa ishara ya nia njema kwa Tehran.Rasoul Movahedian amenukuliwa na gazeti la Financial Times akisema, Iran inataka msaada wa kupata uhuru wa Wairani 5 waliozuiliwa na Marekani nchini Irak.Vile vile ameomba msaada,kupunguza wasi wasi kuhusika na mradi wa nyuklia wa Iran.