1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran itaendelea mbele na mpango wake wa nyuklia

11 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3v

Huku mzozo wa nyuklia wa Korea Kaskazini ukiendelea, Iran imesema tena haitazuiliwa katika mpango wake wa kutaka kutumia teknolojia ya nyuklia.

Kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ametangaza kwamba serikali ya Tehran haitakubali shinikizo la kimataifa.

Badala yake itaendelea mbele na shughuli zake za kurutubisha madini ya uranium, licha ya azimio la Umoja wa Mataifa linaloitaka Iran isitishe urutubishaji wa uranium na vivutio ilivyoahidiwa ikiwa itakubali kuwachana na mpango wake wa nyuklia.