1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran kujiimarisha nchini Irak

29 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWf

Iran imeanza kuchukua hatua za kupanua na kuimarisha uhusiano wake wa kijeshi na kiuchumi na Irak. Balozi wa Iran nchini Irak, Hassan Kasemi Qomi, ameliambia gazeti la New York Times kwamba Iran iko tayari kusaidia kwa kutoa mafunzo kwa jeshi la Irak, walimu na vifaa na pia kuchukua jukumu kubwa katika kuijenga upya Irak.

Mpango huo wa Iran unaweza kuchochea hali ya wasiwasi baina yake na Marekani. Katika majuma machache yaliyopita, Marekani iliwatia mbaroni wanaharakati wa kiiran na inasema Iran imehusika katika mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Marekani na wa Irak.

Qomi alikiri kwamba Wairan waliokamatwa mwezi uliopita walikuwa maofisa wa usalama, lakini akasema walikuwa wakifanya mazungumzo rasmi na maofisa wa Irak kuhusu usalama.