1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Iran yasema itarutubisha zaidi madini ya Urani.

24 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgP

Serikali ya Iran imejibu vikwazo vilivyowekwa na umoja wa mataifa kwa kusema kuwa itaongeza kasi ya kufunga vifaa 3,000 zaidi vya kurutubishia madini ya Urani. Gazeti lenye msimamo mkali nchini Iran la Kayhan limemnukuu mjumbe wa majadiliano ya kinuklia wa nchi hiyo Ali Larijani akisema kuwa shughuli katika kinu cha kurutubishia madini ya Urani cha Natanz itaendelea bila kusita.

Mataifa ya magharibi yanahofia kuwa Iran inaweza kutumia madini ya Urani yaliyorutubishwa kwa kutengeneza bomu la kinuklia.

Iran imekwisha sema hapo kabla kuwa mpango wake huo wa kinuklia ni wa amani, wenye lengo kuu la kuzalisha umeme.

Azimio hilo la umoja wa mataifa linaamuru nchi zote kusitisha kuipatia Iran vifaa vinavyohusika na nuklia pamoja na teknolojia.

Pia azimio hilo linazuwia mali za makampuni 10 muhimu ya Iran pamoja na watu binafsi 12. Iran imelishutumu azimio hilo, na kulieleza kuwa ni kinyume na sheria.