1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Mgawo wa petroli wasababisha vurugu Iran

28 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnj

Hatua iliyochukuliwa na Iran kuanzisha mgawo wa petroli imesababisha hasira na vurugu katika mji mkuu,Tehran.Maafisa wamesema,hadi vituo 19 vya petroli vimetiwa moto na waendesha magari waliohamakishwa,kwa sababu ya kuarifiwa saa chache tu kabla ya hatua hiyo kuingia kazini. Wengi wamemlaani Rais Mahmoud Ahmedinejad,ambae serikali yake tangu majuma kadhaa,ilionya kuwa itaanzisha mgawo wa petroli katika juhudi ya kupunguza athari za vikwazo vya Umoja wa Mataifa, pindi kutawekwa vikwazo dhidi ya maagizo ya mafuta pia.Iran ni miongoni mwa wazalishaji wakuu wa mafuta yasiosafishwa,lakini kwa sababu ya uwezo wake mdogo wa kusafisha mafuta,Iran inapaswa kuagizia kutoka nje,takriban nusu ya mahitaji yake ya petroli.