1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Mwanadiplomosia ametekwanyara nchini Irak

6 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUS

Wizara ya mambo ya kigeni ya Iran imethibitisha kuwa mwanadiplomosia wake mmoja ametekwa nyara katika mji mkuu wa Irak,Baghdad.Vyombo vya habari vimemnukulu msemaji wa wizara ya kigeni akisema kuwa Jalal Sharafi aliekuwa afisa katika ubalozi wa Iran mjini Baghdad,alitekwa nyara siku ya Jumapili na kundi linalohusika na wizara ya ulinzi ya Irak.Akitoa wito wa kumuachilia huru,amesema vikosi vya Kimarekani vina dhima ya kuhakikisha usalama wa mwanadiplomasia huyo.Hapo awali,afisa mmoja wa Kiiraki alisema, mwanadiplomasia huyo alitekwa nyara na watu wenye silaha waliovaa sare ya kikosi maalum kinachofanya kazi na majeshi ya Kimarekani. Utekaji nyara huo umetokea wakati ambapo mivutano inazidi kati ya Marekani na Iran.Washington inaituhumu Tehran kuwa inayasaidia makundi ya wanamgambo nchini Irak,madai ambayo yanakanushwa na Iran.