1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran: Rais wa Syria, Bashar al-Asaad, ziarani Iran

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCR6

Rais Bashar al-Assad wa Syria amewasili Tehran kufanya ziara ya siku mbili ambapo atafanya mazungumzo juu ya hali ya mambo ilivyo katika Mashariki ya Kati. Atakutana na rais wa Iran, Mahmud Ahmadinejad, kiongozi wa kidini, Ayatollah Ali Khamenei, na rais wa zamani, Ali Akbar Rafsanjani. Hali zilivyo huko Iraq na Libanon na ushirikiano pamoja na Wapalastina ndio masuala yanayotarajiwa yatakuweko katika ajenda ya mazunguzo yake. Iran na Syria zimekuwa na maingiliano makubwa tangu rais Ahmadinejad kuingia madarakani. Nchi mbili hizo zimetuhumiwa kuwa zinawaunga mkono waasi katika nchi jirani ya Iraq.