1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Israil yateua waziri wa kwanza mwarabu mwislamu.

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCX0
Rais George Bush wa Marekani akiweka shada la mauwa katika Uwanja palipokuweko Kituo cha Biashara Duniani, New York, kilichoshambuliwa na magaidi wa al-Qaida miaka sita iliopita.
Rais George Bush wa Marekani akiweka shada la mauwa katika Uwanja palipokuweko Kituo cha Biashara Duniani, New York, kilichoshambuliwa na magaidi wa al-Qaida miaka sita iliopita.Picha: AP

Serikali ya Israil imeidhinisha uteuzi wa waziri wa kwanza mwarabu mwislamu nchini humo.

Ralib Majadele wa chama cha Labour ameteuliwa kuwa waziri asiye na wadhifa maalum lakini anatarajiwa kupewa majukumu mengine kwenye mabadiliko yanayotarajiwa kufanyiwa baraza la mawaziri hivi karibuni.

Ralib Majadele amechukua mahali pa waziri wa zamani wa Sayansi, Utamaduni na Michezo Ophir Pines-Paz aliyejiuzulu mwezi Oktoba mwaka uliopita akipinga kujumuishwa chama cha Yisrael B´teinu kwenye serikali.

Ralib Majadele anasema uteuzi wake unatoa nafasi nzuri ya uwakilishi wa jamii ya Waarabu ambao ni asilimia 20 ya umma wa watu milioni saba nchini Israil.

Suala la uteuzi wa Raleb Majadele litawasilishwa bungeni kupata idhini ya mwisho kesho.