1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Polisi yadai rais Moshe Katsav ashtakiwe mahakamani

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2M

Polisi nchini Israeli wamedai rais wa nchi hiyo, Moshe Katsav, afunguliwe mashtaka ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia na ubadhilifu.

Agizo hilo limetolewa katika mkutano kati ya wachunguzi wa polisi na hakimu mkuu wa jamhuri, Meni Mazuz, ambae ndie mwenye kuwa na madaraka ya kuamua ikiwa rais afunguliwe mashitaka au laa. Wakili wa rais Katsav, Zion Amir, amesema polisi hawana mamlaka ya kupeleka mashitaka mahakamani na kukumbusha kuwa kwa muda wote polisi ilijaribu kufanya hivyo, mara nyingi madai yao hayakuzingatiwa.