1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Waziri Jung amekutana na Peretz na Siniora

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwG

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung amekuwa na mazungumzo pamoja na waziri mwenzake wa Israel Amir Peretz mjini Tel Aviv.Wakati wa ziara yake ya Mashariki ya Kati,majadiliano yake yamehusika na ujumbe wa wanajeshi wa Kijerumani kupiga doria nje ya pwani ya Lebanon katika Bahari ya Mediterania.Baada ya kukutana na Peretz,waziri Jung alisema,amehakikishiwa kwamba matukio ya hivi karibuni ambapo ndege za kijeshi za Israel zilifyatulia risasi manowari ya kijeshi ya Ujerumani,hayatorudiwa tena.Hapo awali,waziri Jung alikutana na waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora mjini Beirut.Vikosi vya wanamaji vya Umoja wa Mataifa vinavyoongozwa na Ujerumani, vinalinda pwani ya Lebanon,kama sehemu ya makubaliano yaliyositisha vita vya mwezi mmoja kati ya Israel na Hezbollah.Waziri Jung sasa amewasili Cyprus kutembelea kituo cha vikosi vya Kijerumani katika kisiwa hicho.