1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko kubwa la ardhi laikumba Haiti

Yusra Buwayhid
7 Oktoba 2018

Tetemeko la ardhi limepiga pwani ya kaskazini mwa Haiti. Watu kadhaa wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa. Kumezuka hali ya taharuki katika kisiwa ambacho bado kinapambanana athari za tetemeko la ardhi la 2010.

https://p.dw.com/p/367dF
Karte Infografik Haiti Erdbeben

Watu wapatao 11 wamefariki na mamia wengine wamejeruhiwa baada ya Jumamosi kutokea tetemeko la ardhi la kiwango cha 5.9, katika kisiwa cha Karibi cha Haiti. Watu saba wamefariki katika mkoa wa kaskazini wa Nord-Ouest na mia moja wamefikishwa hospitali, amesema msemaji wa serikali Eddy Jackson Alexis . Wanne wengine wameripotiwa kufariki katika mji wa Gros Morne na wengine wapatao mia moja kujeruhiwa.

Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Rais Jovenel Moise amesema amumtaka Waziri Mkuu Jean-Henry Ceant kuratibu shughuli za uokozi na kuwataka wananchi wa Haiti kwa jumla kuwa na utulivu.

Nchi hiyo maskini ilipigwa na tetemeko la ardhi la kiwango cha 7.0 mnamo mwaka 2010 ambapo zaidi ya watu 220,000 walipoteza maisha.