1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko la ardhi nchini Chile.

27 Februari 2010

Watu 78 wafa baada ya Chile kutingiswa na tetemeko kubwa la ardhi.

https://p.dw.com/p/ME1M
Tetemeko la ardhi Chile, watu 78 wauawa.Picha: AP

Rais wa Chile Michelle Bachelet ametangaza hali ya kitaifa ya janga nchini humo baada ya watu 78 kuuawa  kufuatia tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha richta 8.8  kutokea nchini humo mapema leo. Majengo yaliporomoka katika mji mkuu, Santiago, kilomita 300 kutoka kitovu cha tetemeko hilo. Kulingana na Taasisi ya Jeologia ya Marekani, USSG kitovu cha Zilzala hiyo ilikuwa kilomita 90 kutoka mji wa Concepcion, mji mkuu wa pili nchini Chile. Nchi za eneo la Pacific na mataifa yote 53, katika eneo la pwani ya Magharibi ya Kusini na Amerika ya Kati, yametoa onyo ya kutokea kwa dhoruba la Tsunami.

Chile Erdbeben Februar 2010
Gari zapindukia kwa kishindo cha tetemko la ardhi.Picha: AP

Onyo kama hilo pia limetolewa, nchini Japan, Australia na Alaska nchini Marekani.Ukilinganisha, tetemeko lililotokea kisiwani Haiti mwezi wa Januari  lilikuwa na ukubwa wa 7.0.