1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEXAS:mtu wa mia minne anyongwa Texas

23 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWl

Mtu aliepatikana na hatia ya kuua amenyongwa kwa kudungwa sindano katika jimbo la Texas Marekani.

Mtu huyo Johnny Connor ni wa mia nne kunyongwa tokea adhabu ya kifo irudishwe tena mnamo mwaka 1976 katika jimbo la Texas.

Gavana wa jimbo hilo Rick Perry alitoa ruhusa ya kutekelezwa adhabu hiyo licha ya miito kutolewa na Umoja wa Ulaya kusihi isitekelezwe.