1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbeki awasilisha hati za kujiuzulu.

Mtullya, Abdu Said22 Septemba 2008

Chama kinachotawala nchini Afrika Kusini -ANC leo kinatarajia kumteua kaimu rais baada ya rais Thabo Mbeki kuwasilisha hati za kung'atuka.

https://p.dw.com/p/FMXs
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini .Picha: picture-alliance /dpa

JOHANENNESBURG.


Chama kinachotawala nchini Afrika Kusini  ANC, leo kinatarajia ,kumteua kaimu-kiongozi  baada ya rais Thabo Mbeki kuwasilisha hati  za kujiuzulu.

Chama hicho kilichukua hatua ya kumtoa bwana Mbeki madarakani ili kuutatua mgogoro mkubwa wa kisiasa ambao haujawahi kukikabili chama cha ANC tokea kumalizika mfumo wa kibaguzi nchini  Afrika Kusini.

Chama cha ANC kimemtoa Mbeki madarakani  kabla ya muda wake rasmi wa urais kumalizika hapo mwakani. Hatua hiyo ilichukuliwa siku  nane baada ya  hakimu kutupilia mbali mashtaka ya rushwa dhidi ya kiongozi wa chama hicho bwana Jacob  Zuma.

Katika uongozi wake Mbeki alifanikiwa kudumisha  kipindi kirefu cha  ustawi wa uchumi na alitoa mchango mkubwa katika utatuzi  wa   migogoro kusini mwa Afrika.

Mbeki  amesema anaheshimu  uamuzi wa chama chake na kwamba ataendelea kuwa mwanachama mtiifu.

Habari  zinasema spika wa bunge Baleka Mbete anatazamiwa kuteuliwa kuwa kaimu rais.