1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Thailand-maguruneti yafyetuliwa

Oumilkher Hamidou30 Novemba 2008

Polisi yajaribu kuzungumza na wapinzani

https://p.dw.com/p/G6Cj

Bankok:

Wapinzani zaidi ya 50 wa serikali ya Thailand wamejeruhiwa abaada ya gurumneti kuripuliwa.Shambulio hilo limezidisha makali ya mzozo unaoongozwa na wapinzani wa serikali nchini humo.Jengo la serikali linazingirwa na waafuasi wa upande wa upinzani tangu Agosti iliyopita.Wanadai waziri mkuu SOMCHAI WONGSAWAT ajiuzulu.Miripuko imeripotiwa pia katika kituo cha televisheni cha upande wa upinzani na karibu na uwanja wa ndege wa safari za ndani nchini.Watu wawili wamejeruhiwa.Viwanja vyote viwili vya ndege vinashikiliwa tangu siku kadhaa sasa na wapinzani.Jaribio la vikosi vya usalama kuwatimua wapinzani hao,limeshindwa.Duru za kuaminika kutoka Bankok zinazungumzia  juhudi za polisi kuzungumza na wapinzani ili waondoke salama katika viwanja hivyo vya ndege.Wataalii laki mojua pamoja na wafanyabiashara wamekwama kufuatia kuzingirwa viwanja  vya ndege nchini Thailand.