1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Theresa May aomba radhi kwa viongozi wa nchi za Caribbean

Amina Mjahid
17 Aprili 2018

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ameomba radhi kwa viongozi wa nchi za Caribbean baada ya serikali yake kutishia kuwafukuza Uingereza watu waliyohamia nchini humo miaka ya 1950 na 1960.

https://p.dw.com/p/2wCsI
UK Theresa May entschuldigt sich bei karribischen Staaten für britische Politik gegenüber Migranten
Picha: Reuters/D. Leal-Olivas

Katika mkutano ulifanyika Downing Street Uingereza Waziri Mkuu wa nchi hiyo Theresa May amewaambia wawakilishi wa nchi 12 za Caribbean wanachama wa Jumuiya ya madola kwamba amelizingatia suala la wahamiaji hao kwa umakini mkubwa.

"Na hasa kizazi cha windrush kimesaidia kuijenga nchi tunayoishi leo, nataka kuondoa picha inayodhaniwa kwamba serikali y ngu inajaribu kuwafungia wananchi wa Jumuiya ya madola, hasa wale wa nchi za Caribbean waliyoleta maisha hapa. Nalichukulia suala hili kwa umakini sana.  Nataka kuomba radhi kwenu leo, poleni kwa wasiwasi tuliyowasababishia,"alisema Theresa May.

Serikali ya Uingereza imekosolewa vikali namna ilivyowashughulikia watu waliyohamia nchini Uingereza kati ya mwaka 1948 wakati meli ya Windrush ilipowasili na kundi la kwanza la wahamiaji wa Caribbean mapema 1970 waliyotokea eneo linalojulikana kama West Indies , makoloni ya zamani ya Uingereza katika Carribean.

Wahamiaji hao na wazazi wao walialikwa nchini Uingereza kwa lengo la kusaidia kuijenga upya nchi hiyo baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, wakati wengi wao kihalali walikuwa waingereza baada ya kuzaliwa nchi yao ikiwa chini ya koloni la Uingereza na wakapewa nafasi ya kubakia huko milele.

Syrien - Militärschlag - Theresa May
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May Picha: picture alliance/AP Photo/UK Government

Hata hivyo wale ambao hawakuweza kupata stakabadhi zao halali za kubakia, kwa sasa wanasemekana kuishi nchini humo kinyume cha sheria, hatua inayodhibiti nafasi zao za kazi, kupata huduma za afya na kuwaweka katika hatari ya kufukuzwa, iwapo watashindwa kuthibitisha hali ya maisha yao nchini Uingereza.

Mgogoro huo uliyopo kwa sasa ambapo mbunge mmoja ameutaja kama aibu ya kitaifa ni fedheha kubwa kwa serikali inayoendelea na mkutano wiki hii wa viongozi wa mataifa 53 wa Jumuiya  ya madola mjini London.

Aidha Timothy Harris, Waziri Mkuu wa Saint Kitts na Nevis, ameelezea matumaini yake kwamba Uingereza itafanya jambo la haki ikiwemo kutoa fidia. Naye kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamaica Minister Andrew Holness ambaye awali alikuwa na mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu May amesema angelipenda pawepo na majibu ya haraka.

Hata hivyo Uingereza imewaandikia barua nchi zote za Caribbean kuelezea namna inavyonuia kusawazisha hali, kwa kuwasaidia wale wote waliyoathirika kupata stakabadhi muhimu za kuishi Uingereza. Pia vile vile imeahidi kuondoa malipo yanayohitajika ya kuomba makaazi ya kudumu na kutoa fidia kwa gharama zilizotumika kushughulikia masuala yao ya kisheria.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Gatone Browne alisema hapo mapema , hatua ya kuomba Radhi ya  May inakaribishwa lakini pia amefurahishwa na namna serikali ilivyoingilia kati kusaidia zaidi.

Mwandishi: Amina Abubakar/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman