1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Thomas Schaaf achukua usukani Hanover

28 Desemba 2015

Thomas Schaaf ameteuliwa kuwa kocha wa klabu inayoyumba ya Bundesliga, Hanover kuiongoza klabu hiyo hadi mwaka wa 2017

https://p.dw.com/p/1HUfY
Thomas Schaaf Trainer Frankfurt 16.8.2014
Picha: Imago

Schaaf mwenye umri wa miaka 54, anachukua usukani kutoka kwa Michael Frontzeck, aliyejiuzulu wiki moja iliyopita katika klabu hiyo inayoshikilia nafasi ya pili kutoka nyuma. Hanover imesema kuwa itamzindua kocha huyo mpya mnamo Januari nne wakati mazoezi ya kipindi cha pili ya msimu wa Bundesliga yatakapoanza.

Schaaf alimaliza muda mwingi kama mchezaji wa Werder Bremen na pia akawahi kuifunza timu hiyo kati ya mwaka wa 1999 na 2013, huku akishinda taji moja la Bundesliga na matatu ya shirikisho la Kandanda la Ujerumani – DFB Pokal. Alikuwa pia kocha wa Eintracht Frankfurt ambako alijiuzulu mwezi Mei. Schaaf amesema yuko tayari kwa changamoto mpya inayomkodolea macho.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Mohammed Khelef